MKUU wa wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora Peres Magiri amezindua wa ujenzi wa wodi mbili za wazazi
Na Mussa Mbeho,SIKONGE
MKUU wa wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora Peres Magiri amezindua
wa ujenzi wa wodi mbili za wazazi katika kata ya kitunda ili kuweza kupunguza msongamano wa wagonjwa katika wodi ya akina mama wajawazito kwenye hospitali ya wilaya hiyo.

Akizungumza nara baada ya kuzindua ujenzi wa wodi hizo mkuu wa wilaya ya sikonge Bwana Peresi Magiri amesema kuwa mpango wa ujenzi wa wodi hizo umeanzishwa ili kuboresha huduma za afya kwa mama na mtoto ikiwemo wajawazito na wagonjwa wengine wilayani humo.
Magiri amesema Katika kuunga mkono jitihada za wananchi wa kata hiyo ofisi yake ya mkuu wa wilaya itatoa sh100,000/- ili kufanikisha ujenzi huo.
Nae Afisa Mtendaji wa kata hiyo bwana Ntegwa Machibula amesema ili kufanikisha ujenzi wa wodi hizo mbili na maabara ya somo la fizikia, viongozi na wananchi wa vijiji vyote wamekubaliana kwa pamoja kuchangia jumla ya sh. 34,155,000/- na zoezi la kukusanya michango hiyo bado linaendelea.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho Dk Mussa Maganga amepongeza hatua nzuri iliyochukuliwa na uongozi wa kata hiyo kwa kushirikianana serikali ya wilaya kwani itasaidia kuboresha huduma za afya katika kituo hicho.
Comments
Post a Comment