MGOMBEA UENYEKITI JUMUIA YA VIJANA UVCCM MKOA WA KATAVI AKAMATWA NA KUACHIWA SAATANO USIKU
KATAVI
Uchaguzi wa jumuiya mbalimbali katika chama cha
mapinduzi ccm mkoa wa katavi uliofanyika jana umeingia dosari kutokana na moja
wa aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti UVCCM Benard Nswima kuenguliwa na
kisha kukamatwa na polisi
Bwana Nswima alikamatwa na kisha kuachiliwa huru
saa 5 usiku wa jana baada ya kuhoji kutoonekana kwa jina lake kwenye orodha ya
wagombea ilhali alikwishapokea barua ya uteuzi kutoka katika ofisi yake
Katika utetezi wa sakata hilo Katibu wa UVCCM
mkoa wa Katavi Bwana Abdulkarim G. Halamga amesema hatua ya kumtia nguvuni
Bwana Nswima ilikuja ili kuzuia uchaguzi kutoharibika licha ya kukiri kuwa ni
kweli Bwana Nswima anayo barua inayoonesha kuwa aliteuliwa kugombea
kinyang’anyiro hicho
Uchaguzi huo wa Jumuiya ya Vijana UVCCM
uliofanyika jana bwana Theonas Kinyonto ametangazwa kuwa mwenyekiti mpya huku
bwana Dickson Kevilo akichaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu UVCCM taifa
Katika nafasi zingine bi Feizal Shebidalla
amechaguliwa kuwa mjumbe wa baraza kuu UVCCM na nafasi ya Mkutano mkuu
amechaguliwa Bi Neema Frank Tarimo
Source Haruna
Juma
Editor
Alinanuswe Edward

Comments
Post a Comment