Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa katavi Damasi Nyanda amewataka wananchi kusherekea kwa amani Sikukuu zinazokaribia na kufuata sheria ziliwekwa.
KATAVI
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa katavi Damasi Nyanda amewataka wananchi kusherekea
kwa amani Sikukuu zinazokaribia na kufuata
sheria ziliwekwa.
Ameyasema
hayo wakati akizungumza na Mpanda Redio na kueleza kuwa jeshi la polisi
limejipanga vizuri ili kuhakikisha wananchi wanasherehekea kwa amani bila
kuwepo na uvunjifu wa amani.
Aidha
amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao hasa katika kipindi hiki cha
kuelekea sikukuu na kutoa ovyo kuwa watoto hawaruhusiwi kuingia maeneo ya
disco.
Wananchi
wamekuwa hawaripoti baadhi ya viashiria vya matukio ya uharifu ambayo baadaye
yamekuwa yakisababisha madhara suala ambalo amewataka pia kuripoti taarifa
hizo.


Comments
Post a Comment