Halmashauri ya Mpanda ya kanusha kitisho cha uwepo wa Pembejeo feki za kilimo
Halmashauri ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imekanusha
kuhusu uwepo wa pembejeo feki zinazo sambazwa na kutumika katika msimu huu wa
kilimo.
Hayo yamesemwa na afisa kilimo wa halimashauri hiyo Bw Fabian
Kashindye alipokuwa akizungumza na mpanda radio ambapo ameeleza kuwa kitisho
hicho ni sawa na propaganda.
Zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wa Tanzania hutegemea kilimo
katika kuendesha maisha na kipato cha kaya, wengi wao ni kutoka vijijini ambao
hukabiliwa na elimu duni kuhusu kilimo bora.
Hivi karibuni Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba ameitaja mikoa ya
Rukwa, Njombe, Iringa, Songwe na Mbeya kuongoza kwa kuuza mbegu feki za mahindi
na kusababisha madhara makubwa kwa wakulima, ikiwemo uzalishaji mdogo wa zao
hilo

Comments
Post a Comment