Wananchi watoa tuzo kwa jeshi la polisi


Wananchi wa Kata ya Kawe wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam, wamelishangaza Jeshi la Polisi baada ya kuaandaa tuzo kwa askari polisi ambao wanafanya kazi vizuri zaidi kwenye eneo hilo.

Akiongea na mwandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni, Jumanne Muliro, amesema jambo hilo ni mfano wa kuigwa kwa wengine, na pia limeonyesha faraja na fundisho kubwa kwao jeshi la Polisi.
“Kwanza ni kitu ambacho kimekuwa cha kuigwa, tofauti na mifumo mingine ya kawaida, wamekuwa wakiifanya kwa siri siri wakiangalia huduma ya kipolisi zinatolewaje, wamethamini kazi za polisi na kuona zinafanywa vizuri, wameona nini wafanye, na hii wametufundisha kitu kimoja, kwamba polisi wazuri wanawajua wao na sio sisi”, amesema Kamanda Muliro.
Sherehe hizo za kuwapa tuzo askari hao zinafanyika katika viwanja vya kituo cha Polisi Kawe, na kuhudhuriwa na wananchi wa Kawe na Polisi wa eneo hilo.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.