Mnyeti akana kuita waandishi ofisini kwake leo


Mkuu  wa Wilaya Arumeru, Elexander Mnyeti akana kuita waandishi ofisini kwake leo Jumatatu kujibu tuhuma za rushwa kwa madiwani waliohama Chadema na kujiunga na CCM na yeye akitajwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kuongoza njama hizo   
Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Mnyeti amesema tangu jana baada ya kung'oa jino anaumwa na hajui nani ametoa taarifa kuwa ataongea na waandishi.
"Mimi nikipona ndio nitaongea hizo taarifa za mkutano na waandishi sizijui," amesema. 
Jana kupitia akaunti ya Twitter yenye jina lake alieleza atakutana na waandishi saa sita leo Jumatatu kujibu tuhuma zote huku akieleza video za Nassari sio za  kweli.


Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.