MEYA WA MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVI AZINDUA MRADI WA MAJI YA BURE.



Mstahiki Meya wa manispaa ya Mpanda Wilium Mbogo  amezindua mradi wa maji ya bure unao fadhiriwa na kampuni la  GBP linalojihusisha na uuzaji wa mafuta ya Petrol.

 Akizungumza katika uzinduzi uliofanyika katika kituo cha GBP kilichopo kata ya Majengo mjini Mpanda amewataka wakazi wa eneo hilo kuutumia mradi huo vizuri ili udumu zaidi.

 Kwa upande wa Meneja wa Kampuni la GBP katika kituo hicho amesema kampuni hilo limeamua kutoa huduma ya maji kutokana na kuona adha ya maji inavyo wakabili wakazi wa eneo hilo.

Miongoni wa wananchi walio jitokeza katika hafla hiyo wamesema  mradi huo ni ukombozi kwa akina mama na familia kwa ujumla.

 Mradi huo unatoa zaidi ya lita lakimoja kwa siku ambapo utawanufaisha wakazi wa kata ya majengo na maeneo jirani.



 

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.