JPM AMTOLEA UVIVU MAALIM SEIF









Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa anatambua kuna watu Zanzibar walikuwa wanasubiri kuapishwa baada ya uchaguzi Mkuu 2015 lakini hatambua watu hao wameishia wapi hivi sasa. 

Rais Magufuli amesema hayo leo alipokuwa kwenye kilele cha mbio za Mwenge 2017 shereha ambazo zimefanyika Zanzibar katika uwanja wa amani, Rais Magufuli amedai kuwa watu ambao 
watajaribu kuchezea Muungano wa Tanzania na Zanzibar watashughilika nao kwani wao wataendelea kuupigania Muungano huo ulioasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume.
"Najua huku Zanzibar walikuwepo watu wamejiandaa kuapishwa, sijui wameishia wapi, tutaendelea kuupigania Muungano wetu, na yeyote ambaye atajaribu kuuchezea tutashughulika naye" alisisitiza Rais Magufuli 
Mbali na hilo Rais Magufuli amewataka Watanzania kiujumla kuwa wavumilivu na hali ya uchumi wa sasa na kusema kuwa ni mapito na kuahidi kuwa mambo yatakaa sawa muda si mrefu hata kama hayatakuwa sawa sasa anaamini kuwa watoto na wajukuu wetu watakuja kukuta mambo yako vizuri kwani mageuzi yoyote yale huwa yanachukua muda. 
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ya Urais Zanzibar 2015 baada ya uchaguzi kufanyika alijitangazia matokeo kuwa yeye ndiye mshindi wa nafasi ya Urais kabla ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangaza mshindi. 

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.