Mahakama yafuta matokeo ya uchaguzi wa urais Kenya
MOJA KWA MOJA
Mahakama
ya Juu nchini Kenya imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika
mapema mwezi uliopita katika uamuzi kuhusu kesi iliwasilishwa na muungano wa
upinzani National Super Alliance.
 |
| UHURU KINYATA |
 |
| RAILA ODINGA |
Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa
uchaguzi huo akiwa na kura 8,203,290 (54.27%)
Tume ya uchaguzi ilisema Raila Odinga alipata
kura 6,762,224 (44.74%)
Upinzani unadai mitambo ya tume ya uchaguzi
ilidukuliwa na kuingiliwa kumfaa Rais Kenyatta.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi, kulikuwa na mvutano kuhusu kukaguliwa kwa
mitambo ya tume ya uchaguzi
Mahakama ya Juu inaweza kuidhinisha au kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi.
Iwapo ushindi wa Rais Kenyatta utaishinishwa, basi ataapishwa Septemba 12
Iwapo uchaguzi utafutiliwa mbali, uchaguzi mwingine utafanyika katika
kipindi cha siku 60.
Comments
Post a Comment