HATIMA YA WANAFUNZI WA DARASA LA SABA KATIKA SHULE YA MSINGI NSANDA ILIYOFUTWA KUJULIKANA.
Waliokuwa wanafunzi 10 wa darasa la saba katika shule ya Msingi Nsanda kata ya Kanoge halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi iliyofungwa kwa madai ya kuwa katika hifadhi ya misitu watafanya mtihani wa darasa la saba katika shule ya msingi Kabuga.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nsimbo Filimbi Dipilo alipokuwa
akizungumza na mpanda radio fm kuhusu hatima ya wanafunzi hao, ambapo amesema mkakati
wa maandalizi ume kamilika na kwamba hakuna mwanafunzi atakaye shindwa kufanya
mtihani huo.
Lakini ni takribani mwezi mmoja wanafunzi , hao wanaishi chini ya miti na wazazi familia zao huku wakilalamika kupoteza daftari, na vitendea kazi vingine wakati wa operesheni ya kuondoa makazi katika maeneo hayo.
Kijiji cha Nsanda kipo Kaskazini mwa mkoa wa Katavi umbali wa KM
45 kutoka mji wa Mpanda ambapo wakazi walihamishwa kinguvu ikiwemo kuchomwa
moto kwa makazi yao kwa kile kinachodaiwa kuwa ni eneo la hifadhi ya misitu.
Na Alinanuswe Edward.

Comments
Post a Comment