Posts

 TANZANIA YAENDELEA KUKAA KILELENI Rais wa Tnzania Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania na Romania wamekubaliana kuongeza wigo wa ufadhili wa masomo hususani katika fani za udaktari na ufamasia ambapo Romania imekubali kutoa nafasi kumi (10) za masomo kwa wanafunziwa Tanzania. Rais Samia, akizungumza na waandishi wa habari  leo amesema Serikali za mataifa hayo mawili  zimezungumzia fursa zilizopo katika sekta za afya na utengenezaji wa dawa,kubadilishana uzoefu katika sekta ya kilimo ikiwemo usindikaji wa mazao na kukabiliana na majanga. Wakati huo huo, Tanzania nayo imetoa nafasi tano za ufadhili kwa vijana wa Romania kuja kusoma kwenye vyuo watakavyovichagua ikiwa ni fursa ya kuchangia jitihada za Serikali za kujengea uwezo, rasilimali watu na kuimarisha huduma katika sekta mbalimbali. Akizungumzia mkutano wa mabadiliko ya Tabianchi wa COP28, 2023 Rais Samia amesema Tanzania inatarajia kuweka nguvu suala la nishati na nishati safi ya kupikia, hivyo amemuomba Rais ...

MCHUNGAJI WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA NSIMBO APEWA SAA 24 KUONDOKA

Image
Mchungaji wa Kanisa la ufufuo na Uzima ambaye ni mwangalizi wa kanda ya Nsimbo Lameki Monde aliyedai kufufua marehemu katika Kata ya Stalike amepewa saa 24 za kuondoka katika eneo hilo. Afisa mtendaji wa Kata ya Stalike akizungumza kwa njia ya simu bila kutaja jina lake amethibitisha suala na kusema kuwa limezua taharuki miongoni mwa wananchi. Mchungaji Lameki Monde amesema amealikwa na familia ya Marehemu Raymond Mirambo aliyefariki miezi miwili iliyopita  kifo ambacho mchungaji huyo anasema ni chakutatanisha. Ndugu wa marehemu wanasema waliamua kumuita mchungaji huyo ili afanye maombezi yatakayo saidia kuonekana kimuuujiza kwa mtu huyo. Wakazi wa kata  hiyo wamekumbwa na taharuki hasa kutokana na kuenea kwa taarifa hizo.
Image
Mabomu yanarindima kuwatawanya vijana wenye hasira muda huu ====== Kijana Allen mkazi wa Kata ya Iyela, alikamatwa juzi akiwa na Wenzake aliokuwa akicheza nao Pool Table a taarifa zinadai kuwa alipigwa sana na Askari wa Kituo cha Kati na baada ya hali yake kuwa mbaya leo mchana wakamuachia huru. Ndugu baada ya kuona kijana wao yuko katika hali mbaya walimkimbiza Hospitali ya Rufaa Mbeya ambako jioni ya leo alifikwa na mauti Vijana waliamua kupinga tukio hilo kwa kufunga barabara na hata kuchoma matairi vitendo vilivyopelekea Askari wa Jeshi la Polisi kuwatawanya kwa mabomu ya machozi ambayo bado yanarindima katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Mbeya hadi muda huu(Saa 5 Usiku) Inaarifiwa kuwa mwezi Januari, kijana mwingine kutoka Mtaa wa Airport(Eneo jirani na huyu aliyefariki leo) alifariki saa chache baada ya kuachiwa kutoka Kituo cha Polisi huku ikidaiwa kuwa mauti hayo yalichochewa na kipigo kama huyu wa leo. Wananchi wakidai ni tukio la 4 kutokea

Watanzania wawili kunyongwa China, mtoto arudishwa

Image
Watanzania wawili mume na mke waliotambulika kwa majina ya Baraka Malali na mkewe Ashura Mussa wamekamatwa na dawa za kulevya China katika uwanja wa ndege wa Baiyun Guangzhou wakiwa na mtoto wao mdogo wa miaka 2 ambaye amerudishwa leo nchini Tanzania Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Sheria za Madawa ya kulevya, Edwin Kakolaki amesema kuwa raia hao wa Tanzania Januari 19, 2018 uwanja wa ndege wa Baiyun Guangzhou, wakiwa wamemeza tumboni dawa za kulevya, walihifadhiwa kwenye chumba maalum kwa muda, Baraka alitoa pipi 47 kwa njia ya haja ambapo mkewe alitoa pipi 82. Serikali ya China iliwasiliana na serikali ya Tanzania kuhusiana na suala la mtoto huyo ambapo walikubaliana kumrudisha mtoto huyo nchini, mtoto huyo amewasili leo nchini Tanzania na Serikali kusema kuwa watafanya utaratibu wa kuhakikisha wanawatafuta ndugu wa watu hao ili waweze kuwakabidhi mtoto huyo.  Aidha Kakolaki amewataka Watanzania kuendelea kuwaombea wazazi ha...

Madiwani wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema wamemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aondoke na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bw. Cyprian Luanda baada ya kutoridhishwa na utendaji wake.

Image
Madiwani wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema wamemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aondoke na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bw. Cyprian Luanda baada ya kutoridhishwa na utendaji wake. Wametoa ombi hilo leo katika kikao cha Waziri Mkuu na watumishi Halmashauri ya Buchosa akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza. Waziri Mkuu baada ya kupokea ombi hilo amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongella kwenda katika halmashauri hiyo na kufanya kikao cha pamoja kati ya Madiwani, Mkurugenzi na watumishi ili kubaini changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi. Mbali na hayo Mh. Majaliwa ameweka jiwe la msingi la hospitali ya Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, ambapo ujenzi wake hadi kukamilika unatarajiwa kugharimu sh. bilioni 10.55. Pia Waziri Mkuu amezindua madarasa manne ya Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Secondari ya Nyehunge wilayani Sengerema na kuwataka wanafunzi wasome kwa bidii...

Tanzania yachoma vifaranga wengine 5000 kutoka Kenya

Image
Tanzania kwa mara nyengine tena imechoma vifaranga 5,000 vya kuku vinavyodaiwa kuingizwa nchini humo kupitia mpaka wa Kaskazini wa Namanga kutoka Kenya. Kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya, katibu katika wizara ya mifugo nchini Tanzania Maria Mashingo, amesema kuwa mfanyibiashara aliyeingiza vifaranga hao nchini Tanzania hakuwa na vibali vinavyohitajika . Tanzania imesema kuwa hatua ya kuwachoma kuku hao inalenga kuzuia kuenea kwa homa ya ndege. ''Hakuna haja ya kuathiri sekta yote ya kuku kwa sababu ya vifaranga 5000'', Mashingo alinukuliwa na gazeti hilo akisema. Takriban miezi mitatu iliopita, Tanzania ilichoma vifaranga 6,400 vya kuku wenye thamani ya shilingi 577,000 waliopatikana katika mpaka huohuo , hatua ilioshutumiwa na wanaharakti wa wanyama kutoka mataifa yote mawili. Uamuzi huo pia ulisababisha vita vya kibiashara kati ya mataifa hayo jirani. Source BBC

Chama cha Wafanyakazi chamjia juu Makonda

Image
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) kimelaani kitendo kikichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda cha kuwavua madaraka hadharani watumishi na kusema ni kitendo cha kinyama alichofanya.  Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU), Rashid Mtima amesema hayo leo Februari 13, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kitendo kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa si cha kiuungwana. "Tunacholani ni kitendo cha Mkuu wa Mkoa akiwa kwenye mkutano wa hadhara kuhukumu watendaji wa Serikali za Mitaa hiyo haipo kisheria na tunaomba na kuwataka wanasiasa wafuate utaratibu katika kusimamia nidhamu ya watumishi. Sisi tunatambua na kusema kama chama kitendo alichofanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam si tu cha kinyama lakini kimewadhalilisha watumishi wetu kwenye Serikali za Mitaa na imeonyesha kutoheshimiwa kwa utawala bora wa kisheria kinyume na haki za binadamu"  alisisitiza  ...