MCHUNGAJI WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA NSIMBO APEWA SAA 24 KUONDOKA
Mchungaji wa Kanisa la ufufuo na Uzima ambaye ni mwangalizi wa kanda ya Nsimbo Lameki Monde aliyedai kufufua marehemu katika Kata ya Stalike amepewa saa 24 za kuondoka katika eneo hilo. Afisa mtendaji wa Kata ya Stalike akizungumza kwa njia ya simu bila kutaja jina lake amethibitisha suala na kusema kuwa limezua taharuki miongoni mwa wananchi. Mchungaji Lameki Monde amesema amealikwa na familia ya Marehemu Raymond Mirambo aliyefariki miezi miwili iliyopita kifo ambacho mchungaji huyo anasema ni chakutatanisha. Ndugu wa marehemu wanasema waliamua kumuita mchungaji huyo ili afanye maombezi yatakayo saidia kuonekana kimuuujiza kwa mtu huyo. Wakazi wa kata hiyo wamekumbwa na taharuki hasa kutokana na kuenea kwa taarifa hizo.